MATOKEO YA JANA EPL, CHELSEA WAIKUTA MANCHESTER UNITED KWA ALAMA


Kwa mara ya kwanza katika historia, Willian amehusika katika mabao 3 katika mechi moja akiassist mabao ya Pedro na Bakayoko huku akifunga bao moja na kuifanya Chelsea kuibuka kidede kwa mabao 3 kwa 1.


Kwa matokeo  hayo Chelsea wamefikisha alama 35 sawa na Manchester United lakini Chelsea wanakuwa wamezidiwa idadi ya mabao ya kufunga huku wakiwa wametangulia mchezo mmoja.
Crystal Palace waliipiga Watford mabao mawili kwa moja, huku Julian Speron wa Crystal Palace akicheza mchezo wake wa 400 tangu ajiunge na na klabu hiyo tarehe 14/08 mwaka 2014 huku Watford wakimaliza pungufu baada ya Tom Clevery kupewa kadi nyekundu.
Stoke City ambao wiki iliyopita walizomewa na mashabiki wao kutokana na kiwango kibovu wameendelea kuboronga baada ya kufungwa bao moja kwa nunge na Burnley kwa bao lililofungwa na Ashley Barnes.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.