MAN CITY WAHARIBU REKODI NZURI YA UNITED NDANI YA OT, CITY NJIA NYEUPE UBINGWA

Baada ya safari ndefu ya michezo 40 bila kupoteza katika uwanja wao wa Old Traford hatimaye Jose Mourinho ameambulia kipigo katika uwanja huo baada ya Man City kuwafunga bao 2 kwa 1.
Huu ulikuwa mchezo wa 20 kati ya Pep Gurdiola na Jose Mourinho huku Pep Gurdiola anaendeleza ubabe wake kwa Mourinho kwani baada ya mchezo wa leo Pep anakuwa amemfunga Mou mechi 10 katika mechi hizo 20.

City walionekana kuliandama sana goli la Manchester United kipindi cha kwanza na dakika ya 43 David Silva alitumia makosa ya Romelu Lukaku na kuiandikia City bao la kuongoza kabla ya Rashford kusawazisha dakika chache baadae.
Kipindi cha pili United walionekana kutulia lakini makosa ya uokoaji ya Lukaku tena yalitumiwa vyema na Manchester City na mlinzi wao Nicolas Otamendi akaiandikia City bao la pili na la ushindi.
Matokeo ya leo yanawapa City nafasi kubwa kuchukua ubingwa wa EPL msimu huu kwani kwa sasa pengo la alama kati yao na Manchester United linaongezeka hadi kufikia alama 11 huku zikiwa zimebaki mechi 3 kwa raundi ya kwanza kuisha.
Matokeo mengine ya jana EPL ni kama yanavyo onekana hapo chini



No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.