HIZI NDIZO RECORD 5 AMBAZO MESSI AMEWEKA BAADA YA EL CLASICO




Klabu ya Barcelona imeendelea kujichimbia kileleni mwa La Liga baada ya kuichakaza Real Madrid goli 3-0 katika El Clasico mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.



Mchezo huo wa El Classico uliokuwa wa kuvutia hadi mapumiziko hakukuwa na mbabe aliyegusa nyavu za mwenzake. Kipindi cha pili kilikuwa kichungu kwa Madrid ambayo ilikubali mabao mawili ya Luis Suarez na Lionel Messi aliyefunga kwa mkwaju wa penalti huku Madrid ikicheza pungufu baada yabeki wake wa kulia, Dani Carvajal kulambwa kadi nyekundu baada ya kuunawa mpira makusudi akiuzuia usitinge wavuni.

Wakati hayo yakijiri Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi kwenye mchezo huo ameweka rekodi tano kupitia mchezo huo.



1-Messi anakuwa mchezaji wa Kwanza kufunga magoli 15 dhidi ya Madrid kwenye uwanja wao wa Santiago Bernabeu.
2-Messi anakuwa mfungaji wa muda wote wa El Clasico kwa kufikisha magoli 25 kwenye mechi zote za El Clasico alizocheza hakuna mchezaji aliyewahi kufanya hivyo.
3-Kupitia mchezo huo Messi amevunja rekodi ya Mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich, Gerd Muller ya magoli 525 ambapo Messi kwa ushindi wa leo amefikisha goli 526 na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli mengi akiwa na klabu moja.
4-Messi leo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoa pasi za mwisho (assists) 14 kwenye mechi za El Clasico.
5-Messi ndiye mchezaji pekee wa La Liga aliyetengeneza nafasi nyingi za magoli (9) dhidi ya Real Madrid kwa msimu huu

Kwa sasa Klabu ya Barcelona inaongoza kwenye msimamo wa La Liga kwa alama 14 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid wenye alama 31 wakiwa nafasi ya 4.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.