CHELSEA YAIKARIBIA MAN U, TOTTENHAM NA LIVERPOOL ZAFANYA KWELI, MATOKEO YOTE YA JANA EPL HAYA HAPA



Pamoja na ubora wote lakini huwezi kuamini kwamba hii leo ilikuwa mara ya kwanza kwa Jesse Lingard kufunga mabao akitokea benchi baada ya kufunga mabao mawili yaliyowafanya United kumaliza mchezo kwa sare ya mbilimbili.
Lakini ukiacha bao la kwanza la Burnley, lile la pili lililofungwa na Steven Defeour lilikuwa ni bao la kwanza kwa golikipa wa Manchester United David De Gea kufungwa nje ya eneo la box msimu huu.

Mapema kabla ya mchezo kati ya Manchester United na Burnley, Tottenham waliifunga Southampton mabao 5 kwa 2 huku Harry Kane akifunga Hat Trick yake ya 6 kwa mwaka huu wa 2017.
Cezar Azzipuculeta alitoa assist ya 6 kwa Alvaro Morata akafunga bao lake la 11 la kichwa msimu huu ikiwa ni mabao mawili zaidi ya mchezaji yoyote EPL huku bao la pili la Chelsea likifungwa na Marco Alonso huku Brighton wakitoka kapa.


Tom Ince alitoa nuksi kwani kabla ya mechi ya leo alikuwa mchezaji aliyekuwa akishikilia rekodi ya mashuti mengi bila bao(45) na shuti la leo lilikuwa shuti lake la 46 na akafunga bao lililowafanya Huddersfield kutoka suluhu ya moja moja na Stoke City.
Kwa matokeo ya leo nafasi nne za juu Manchester City wanaongoza wakifuatiwa na United huku Chelsea sasa wakiikaribia United ambapo sasa wanakuwa wametofautiana kwa alama moja tuu.

Matokeo mengine ya EPL siku ya boxing day ni kama inavyo onekana hapo chini







No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.