AZAM YAONGOZA LIGI, RATIBA YA VPL LEO JUMAMOSI



Azam wameiteka nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Stand United, ushindi huo umewafanya wafikishe pointi 26 na kuidizi Simba kwa pointi tatu lakini Azam wakiwa mbele kwa mchezo mmoja.
Simba itacheza kesho Jumamosi December 30, 2017 dhidi ya Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara ambapo kama watashinda watarejea kwenye nafasi ya kwanza kwa tofauti ya magoli dhidi ya Azam huku wakifungana kwa pointi lakini tofauti na matokeo ya ushindi watawaacha Azam wakitamalaki.
Kwa mara ya kwanza Azam imeshinda kwa magoli zaidi ya moja (Azam 3-0 Stand United) msimu huu wa ligi, kabla ya mchezo huo Azam ilikuwa ikifunga goli moja katika mechi zote walizofanikiwa kufunga.
Mbio za ubingwa wa VPL msimu huu
Wadau wengi wa soka hawaizungumzii sana Azam katika mbio za ubingwa wa ligi kwa msimu huu lakini wamo tena kwa vitendo. Azam wanafukuza mwizi kimyakimya, moja ya vitu amvavyo vinaweza kuwa silaha kubwa kwa benchi la ufundi la timu hiyo ni kurejea baadhi ya nyota wao ambao walikuwa majeruhi (Shaaban Idd, Stephen Kingue) na kuendelea kukipa nguvu kikosi cha Azam.
Kuna baadhi ya watu walishangazwa Himid Mao kuchezeshwa kama mlinzi wa kulia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin na baadhi ya mechi za mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup lakini leo akiwa Azam ameanza katika nafasi ya ulinzi wa kulia akichukua nafasi ya baada ya kukosekana kwa Daniel Amoah ambaye tumezoea kumuona akicheza katika eneo hilo. Hii ni tafsiri kwamba wana watu ambao wanaweza kucheza katika nafasi tofauti na kuisaidia timu kupata matokeo.
Himid Mao si mgeni katika nafasi za ulinzi unaweza kumuona akicheza kwa utulivu na kuisaidia timu yake kupata matokeo.
Kuna wengine huenda wakabeza ushindi wa Azam kwa Stand kwa kigezo kwamba, Stand haifanyi vizuri mzimu huu na imekuwa ikigawa pointi kwa timu nyingine kutokana na udhaifu wa kikosi chao. Unapohitaji ubingwa lazima ucheze mechi zote kama fainali bila kujali unapambana na adui wa aina gani, Azam wameonesha hilo.
Bernard Athur amefunga katika mechi yake ya kwanza VPL, hii inaonesha ni kwa namna gani Azam inafaidika na uwepo wa wachezaji wengi wanaounda kikosi kipana.

RATIBA YA LEO VPL


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.