EMMANUEL OKWI ATWAA TUZO.... SOMA ZAIDI HAPA



Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda anayeichezea club ya Simba SC ya Tanzania Emmanuel Okwi leo September 14 2017 ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi August wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara.
Okwi ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya kufanikiwa kuwashinda kiungo wa Mtibwa Sugar Mohammed Issa aliyesaidia timu yake kupata pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United na Boniface Maganga wa Mbao FC.

Mchezaji huyo alifanikiwa kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya kamati ya tuzo ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia mapendekezo kutoka kwa makocha wa viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.