BREAKING NEWS : LISSU APIGWA RISASI ZAIDI YA 2 AKITOKEA BUNGENI DODOMA MUDA HUU

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu  baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.











Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa amweetoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa ajili ya kufahamu taarifa zaidi.


Na hii ndio gari iliyo shambuliwa kwa risasi akiwemo mhrshimiwa LISSU



No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.