UTABIRI WA ALLY MAYAY TEMBELE KUEKEKEA MCHEZO WA LEO, SIMBA VS YANGA





Mchambuzi wa soka Ally Mayay Tembele amesema, mchezo wa Simba vs Yanga wa August 23, 2017 utakuwa ni mchezo naowahusu makocha zaidi kuliko wachezaji. Kwa mujibu wa 
mtazamo wa Mayay, anaona makocha hawatakuwa na visingio vyovyote kwa wachezaji baada ya kupoteza mechi hiyo bali wao ndio wenye changamoto
“Changamoto kubwa ipo kwa makocha Joseph Omog kwa upande wa Simba na George Lwandamina kwa Yanga, kwa sababu kila timu ina changamoto zake. Angalau  walipata pre-season  nzuri Afrika Kusini ukilinganisha na Yanga, lakini kusajili wachezaji wengi licha ya kuwa wazoefu bado ni changamoto. Unaweza kuwa umesajili wachezaji wengi lakini hujatengeneza timu.”
“Wapo wachezaji wengi akina Okwi, Niyonzima, lakini bado kutengeneza combination inahitaji mda. Hii ndio changamoto aliyonayo mwalim Joseph Omog. Ni kweli amesajili wachezaji ambao unaona Simba inataka matokeo, kwa muda mrefu wamekuwa wakicheza mpira lakini matokeo hawayapati ndio maana hawajashiriki michuano ya kimataifa kwa miaka minne.”
“Kwa hiyo usajili wao wa mwaka huu unaonesha kwamba wamesajili kwa ajili ya kupoata matokeo ndio maana wameshukua wachezaji wenye uzoefu sasa changamoto kubwa aliyonayo Omog ni kutengeneza timu.”
“Kwa upande wa George Lwandamina msimu uliopita alisema anajifunza  na ni kweli amejifunza kwa sababu hakufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa lakini katika msim huu hawezi tena kusema anajifnza tayari anatakiwa atoe matokeo kama alivyofanya akiwa Zesco United.”
“Changamoto kubwa kwake ni kwamba kwa misimu miwili, Yanga imekuwa ikitegemea upande wa kulia kwa zaidi ya asilimia 90 shindi wa Yanga umekuwa ukipitia kwa Simon Msuva au Juma Abdul. Sasa upande ule kwa sasa hivi haufanyi kazi kama ulivyokuwa unafanya kazi misimu miwili iliyopita kwa sababu Simon Msuva hayupo sasa ili akina Tambwe na Ngoma wapate mipira kama alivyokuwepo Msuva ndio changamoto kwa Lwandamina.”
“Kwa siku za hivi karibni ukiangalia mechi ambazo Vicent Bossou hajacheza bado kumeonekana kuwa na changamoto bado hajatengeneza combination kama ilivyokuwa ya wakati ule kutoka nafasi ya ulinzi hadi ya midfield.”
“Ukiangalia kwa mtazamo huo, utaona changamoto kubwa iliyopo ni kwa makocha zaidi kuliko kwa wachezaji. Kumbuka mechi hii ni ya Ngao ya Jamii mechi ambayo ndio inafungua ligi, kwa Simba au Yanga atakaemshinda mwenzake, atakuwa vizuri kisaikolojia kuanza vizuri msimu wa ligi.”
Mayay alikuwa mchezaji wa Yanga na timu ya taifa kabla ya kustaafu na kuendelea na maisha mengine ikiwemo uchambuzi wa masuala ya soka ndani na nje ya nchi.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.