MKOGWE ULIMBOKA MWAKINGWE KAMFUNGUKIA OMOG KUELEKEA MCHEZO WA NGAO YA JAMII BAINA YA SIMBA vs YANGA
Zimebaki siku 4 tu tushuhudie mchezo wa kuashairia Ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Msimu wa 2017/2018 kati ya Simba na Yanga, tarehe 23 August 2017 Jumatano hii Pale Taifa.
Wakati presha ya mchezo huo ikipanda kwa baadhi ya mashabiki wa timu hizo, Mkongwe wa Simba, Ulimboka Mwakingwe ambaye aliichezea Simba kwa mafanikio ameibuka na kumtaka Kocha Joseph Omog kuwa makini na safu yake ta Ushambuliaji.
Ulimboka alisema ameshtushwa na hatua ya washambuliaji wa Simba kufunga mabao machache katika mechi za kirafiki walizocheza nazo, Ulimboka aliyasema haya kabla ya Simba kucheza na Gulioni jana na kushinda kwa goli 5-0 na kumtaka kocha Joseph Omog kulifanyia kazi eneo hilo.
“Sielewi ni mipango ya kocha au la, lakini msimu uliopita Simba walikosa ubingwa kwa idadi ndogo ya magoli, mwalimu aliangalie hilo,” alieleza Mwakingwe.
Mashabiki wa Simba wameingiwa na hofu baada ya safu ya ushambuliaji kufunga mabao matano katika mechi nne za kirafiki ilizocheza dhidi ya Orlando Pirates, Bidvest Wits, Polisi Dar, Mtibwa Sugar, Rayon Sports na Mlandege kabla ya kuivaa Gulioni Fc na kushinda kwa goli 5-0
Baada ya kuongelea safu ya Ushambuliaji, Ulimboka alisema hana wasiwasi na safu ya ulinzi aliyodai itahimili vishindo vya washambuliaji wa timu pinzani kwa msimu huu.

No comments