Mchezo ambao Man City walianza kwa kasi sana na kuutawala huku wakicheza katika dimba lao la nyumbani la Etihad mbele ya umati mkubwa wa mashabiki wao.
Lakini mbwembwe na ubora wa Man City ulizimwa dakika ya 35 na mchezaji wa zamani wa Manchester United bada ya kufunga bao la kwanza kwa Everton.
Bao la Rooney lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinaisha huku City wakienda mapumziko wakiwa wako pungufu baada ya Kyle Walker kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 44.
Bao la Wayne Rooney limemfanya kufikia rekodi ya Allan Shearer ya ufungaji katika ligi kuu nchini Uingereza ya Epl ya kufunga mabao 200+ katika ligi hiyo.
Kipindi cha pili Man City walionekana kutaka kusawazisha bao na mungu si Athumani kwani zikiwa zimesalia dakika 6 mchezo kuisha Raheem Sterling aliisawazishia City na hili likiwa goli la kwanza kwa Sterling kuifunga City.
Kivutio kati mchezo huo alikuwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho aliyekuwa amepigilia kapelo huku akifuatilia kwa makini mchezo wa majirani zake hao.
No comments