MADRID YAIUA VIBAYA BARCA, NEYMAR ASHANGILIA UFARANSA {+ VIDEO }




Mchezo mkubwa siku ya leo ulikuwa nchini Hispania ambapo kulipigwa mtanange wa kwanza wa fainali ya Spain Super Cup na ilikuwa El Classico ukiikutanisha miamba miwili ya Barcelona na Real Madrid.
Mchezo ulionekana mgumu kwa pande zote huku watu wakitaka kuona Barca watakuwaje bila Neymar na dakika ya 50 mlinzi wa Barca Gerrard Pique aliipatia Madrid bao la kuongoza baada ya kujifunga.


Dakika ya 77 Lioneil Messi aliipatia Barca bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati lakini dakika ya 80 Ronaldo aliipatia Madrid bao la 2 kabla ya dakika ya 82 kupewa kadi nyekundu na dakika ya 90 Asensio aliiandikia Madrid bao la 3.

Kule Ufaransa mshambuliaji mpya wa Psg Neymar Dos Santos ameanza kuifungia Psg katika ushindi wa mabao 3 dhidi ya Guingamp huku mabao mengine ya Psg yakifungwa na Edson Cavanni na Jordan Ikoko akijifunga.

Lazio wakiwa ugenini waliifunga Juve 3 kwa 2 huku Alessandro Mugia, Cirro Imobile aliyefunga mara mbili huku yale ya Juventus yakifungwa na Paulo Dyabala.



No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.