HUYU NDIYE RAISI MPYA TFF, KARIA



Kutoka mjini Dodoma katika ukumbi wa St Gasper ulipofanyika mkutano mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Revocatus Kuuli ametangazwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa TFF kwa wajumbe, makamu na Rais wa TFF.
Aliyekuwa makamu wa Rais na kaimu wa Rais wa TFF Wallace Karia ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa TFF kwa kupata jumla ya kura 95 na kuwashida Ally MayayEmmanuel KimbeShija RichardIman Madega na Fredrick Mwakalebela.

Kutoka kulia ni Wallace Karia akiteta jambo baada ya kutangazwa mshindi wa Urais wa TFF
Kwa ushindi huo sasa rasmi Wallace Kariaatatawala nafasi ya Rais wa TFF hadi 2021 makamu wake akiwa ni Michael Richard Wambura aliyewashinda wagombea wenzake wengine watano.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.